Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Wadhifa wa waumini vitani wanapokutana na maadui na makafiri wa Kizayuni, kwa mtazamo wa Qur'ani upo wazi sana.
Miongoni mwa nyadhifa hizo ni kama ifuatavyo:
- Kuthibiti imara
- Kuwa na mafungamano na Mwenyezimungu
- Kutii maamrisho ya kiongozi
- Kutotofautiana wenyewe kwa wenyewe
- Kuwa na istiqama
{یَـٰۤأَیُّهَا ٱلَّذِینَ ءَامَنوا۟ إِذَا لَقِیتُم فِئَةࣰ فَٱثبتُوا وَٱذكُرُوا۟ ٱللَّهَ كَثِیرا لَّعَلَّكُم تُفلِحُونَ. وأَطِیعُوا۟ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَلَا تَنَـٰزَعُوا۟ فَتَفشَلُوا۟ وَتَذهَبَ رِیحُكُم وَٱصۡبِرُوۤا۟ۚ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلصَّـٰبِرِینَ.}
Enyi mlio amini! Mkikutana na jeshi, basi kueni imara, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu sana ili mpate kufanikiwa. Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri. [Surah Al-Anfāl: 45-46]
Tawhidi katika Jihadi
{فَلَم تَقتلُوهُم وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ قَتَلَهُم وَمَا رَمَیتَ إِذۡ رَمَیتَ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ رَمَىٰ وَلِیُبلِیَ ٱلمؤمِنِینَ مِنهُ بَلَاءً حَسَنًا إِنَّ ٱللَّهَ سَمِیعٌ عَلِیم.}
Hamkuwauwa nyinyi lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye wauwa. Na wewe hukutupa, walakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye tupa, ili awajaribu Waumini majaribio mema yatokayo kwake. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Msikizi na Mjuzi. [Surah Al-Anfāl: 17]
Maoni yako